BAADA ya kuenea kwa taarifa kwamba Simba inasaka kwa udi na uvumba saini ya mshambuliaji Mganda Dan Sserunkuma kutoka Gor Mahia, klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Kenya (KPL) imekata mzizi wa fitna kwa kuamua kuongeza muda wa mkataba wa nyota huyo kukipiga nchini humo.
Katibu Mkuu wa Gor Mahia, Chris Omondi amekaririwa leo Jumatano na mtandao wa futaa.com akieleza kuwa wamefungua mlango wa mazungumzo na nyota huyo aliyetwaa kiatu cha mfungaji bora wa KPL msimu huu ili wamwongeze muda wa mkataba wake kubakia katika timu yao.
sere
Omondi amesema Sserunkuma, mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’, ameonesha nia ya kurefusha mkataba wake wa kukipiga na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Kenya.
“Tuko katika mazungumzo naye na ameonesha nia thabiti ya kuendelea kubaki katika timu yetu. Anajua kilichpo mezani na tunajua ni mchezaji muhimu; hivyo hapo ndipo tulipo kwa sasa,” amesema.
Sserunkuma, ambaye alijiunga na Gor Mahia akitokea Klabu ya Nairobi City Stars katikati ya mwaka 2012, alitia kambani mabao 16 msimu huu na kuiwezesha Gor kutetea taji lake la KPL.
 
Top