Na baraka Mbolembole, Dar Es Salaam,
Yanga SC haiku tayari kupoteza mchezo wa Nani Mtani Jembe kwa mara ya pili mfululizo dhidi ya mahasimu wao Simba SC. Mahasimu hao wa soka nchini hawajafungana katika michezo miwili waliyokutana mwaka huu katika ligi kuu Tanzania Bara. Timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa mwisho msimu uliopita mwezi April, pia zilitoka suluhu katika mchezo wa mzunguko wa kwanza msimu huu mwezi uliopita.
Mchezo wa hisani ambao huandaliwa na wadhamini wa timu hizo, Bia ya Kilimanjaro utapigwa Desemba 13 katika uwanja wa Taifa. Yanga ambao walitoa mapumziko ya siku kadhaa kwa wachezaji wake baada ya kusimama kwa muda ligi kuu Bara, itaanza mazoezi yake kujiandaa na mchezo huo wa Mtani Jembe pamoja na michuano ya ligi kuu na ile ya Kombe la Shirikisho barani Afrika. Timu hiyo itaingia kambini Novemba 24 na itaanza kusimamiwa na Walimu wasaidizi, Mbrazil, Leonard Leiva na Mzawa, Salvatory Edward.
“ Tutatanza rasmsi mazoezi yetu 24 Novemba chini ya walimu wasaidizi, Leiva na Salvatory wakati tukimsubori Maximo ambaye atarejea nchini siku chache baada ya kuanza mazoezi. Wachezaji wote tumewapa taarifa kuwa wanatakiwa kuwa tayari wameripoti siku ya Jumamosi ( kesho kutwa). Tunaanza mazoezi rasmi ya mchezo wa Mtani Jembe na lengo letu ni kulipa kisasi cha kufungwa mabao 3-1 mwaka uliopita” anasema meneja wa timu hiyo, Salehe Hafidh.