Tangu alipoondoka kocha Sir Alex Ferguson kwenye uongozi wa benchi la ufundi la Manchester United – klabu hiyo imekuwa katika anguko.
Bado wana nguvu, wanasajili wachezaji wenye majina makubwa, lakini bado wanaweza kuwapoteza wachezaji wao muhimu. Ingawa hatma ya David De Gea baada ya mkataba wake kuisha inaweza ikawa mwanzo wa mabadiliko.
Anamaliza mkataba wake wakati wa kiangazi mwaka 2016, hii inamaanisha kwamba United watahitaji De Gea asaini mkataba mpya kabla ya mwanzo mwa msimu ujao.
De Gea anajua Madrid wanamhitaji, timu hiyo muda mrefu sasa inatajwa kuwa sokoni kutafuta gpolikipa mrithi wa Iker Casillas, anayekaribia mwisho wa uwezo wake. Ikiwa De Gea ataendelea kubaki Old Trafford itakuwa ni mwanzo mzuri wa mabadiliko kwenye klabu.
De Gea sio Cristiano Ronaldo. Kuichezea Real Madrid haijawahi kuwa ndoto yake. Ni mtoto wa Atletico Madrid, klabu iliyomlea tangu alipokuwa na miaka 10 mpaka aliposajiliwa kwa £18m miaka 11 ijayo.
Mara nyingi, makuzi ya vijana waliolelewa na kwenye utamaduni wa Atletico wamekuwa na wagumu kwenda kuichezea Real Madrid, Fernando Torres alishawahi kusema kwamba hatokuja kuichezea Madrid hata kwa ofa nzuri kiasi gani.
Kumpoteza De Gea ambaye kwa sasa anaelekea kwenye level ya juu ya kiwango chake, itakuwa ni pigo kubwa kwa United na itamaanisha kwamba wamepoteza nguvu ya kuzuzia wachezaji wao kutogusika.
Katika mbio ndefu mpaka kufikia mwisho wa msimu huu, Lousi Van Gaal itabidi ahakikishe kwamba timu iwe imerudi kwenye hadhi yake kwa maana ya nafasi nne za juu. Msimu ujao ni lazima timu ishiriki michuano ya ulaya.
 
Top