Winga wa Yanga Simon Msuva amesema hana mpamgo wa kuachana na timu yake anayoichezea kwa sasa na kujiunga na klabu za Simba na Azam kwakuwa ziliwahi kumdhalilisha siku za nyuma, Goal imegundua.
Msuva ambaye kwa sasa yupo Afrika Kusini na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Satars’ wakijiandaa na mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Swaziland itakayo chezwa Jumapili Novemba 16 amesema ataendelea kuichezea Yanga hadi atakapo staafu kucheza soka kwa vile ni timu anayoipenda toka moyoni mwake.
“Nimewahi kucheza Azam tangu timu ya vijana lakini viongozi walinitoa kwa madai sina kiwango nikapelekwa kwa mkopo timu ndogo ya Moro United lakini hata Baba aliwahi kunipeleka Simba ili nikaichezee lakini viongozi wao Ismail Aden Rage na Makamu wa Rais aliyepo madarakani kwa sasa Geofrey Nyange Kaburu walinikataa wakidai sina uwezo wa kuichezea timu kubwa kama Simba,”amesema Simon Msuva akiongea na Goal.
Simon Msuva amesema kwa sasa hana mpango wa kuiacha Yanga na ataendelea kuutumikia mkataba wake wa miaka miwili na pindi utakapo malizika ataongeza tena kwa sababu anajisikia mwenye furaha kuendelea kucheza timu hiyo yenye historia kubwa katika soka la Tanzania.
 
Top