Man United agree permanent €56 million Falcao deal
Mhariri mkuu wa gazeti la Daily mail Ian Ladyman ni mwandishi wa habari ambaye sifa ya kuripoti habari nyingi zenye ukweli hasa zinazoihusu Manchester United.
Leo hii kupitia gazeti hilo Ladyman ameandika habari juu ya uhamisho wa kudumu wa Radamel Falcao kutoka Monaco kwenda Manchester United.
Kwa mujibu wa Dailymail leo ni kwamba Manchester United Louis van Gaal tayari ameanza kuwa na mashaka juu ya hali ya kiafya ya Falcao na uwezo wake wa kucheza kwenye Barclays Premier League – ligi ambayo inasifika kwa matumizi makubwa ya nguvu katika staili ya uchezaji.
United walimsajili mshambuliaji huyo wa Colombia kwa mkopo kutoka Monaco mwanzoni mwa msimu huu na tayari dili la kudumu lipo katika hatua ya mwisho kukamilika ikiwa tu atafanya vizuri katika msimu huu.
Hata hivyo, Falcao ambaye alikuwa akisumbuliwa na majeruhi ya goti msimu uliopita mpaka sasa ameanza kwenye mechi 3 tu kati ya 10 huku akiwa anasumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28, kwa sasa anauguza jeraha la paja alilopata mazoezini siku mbili kabla ya mchezo wa Chelsea.
Falcao amefanikiwa kufunga goli moja na Van Gaal pamoja na jopo lake la makocha wanaripotiwa kumuweka kwenye uangalizi Falcao wakihitaji kuona mabadiliko makubwa katika afya yake kuanzia sasa mpaka mwishoni mwa msimu ili kumhakikishia usajili wa kudumu.
United wameshindwa kutoa uhakika wa dili la kudumu kwa mchezaji ambaye ni injury prone huku akielekea kutimiza miaka 29 hivi karibuni, mpaka pale watakapopata uhakika wa hali yake.
 
Top