Kiungo mkabaji Emerson De Oliveira Neves Roque leo amesaini mkataba
wa mwaka mmoja kuitumikia Yanga baada ya benchi la ufundi kuridhika na
uwezo wake na mchezaji mwenyewe kufikia makubaliano hayo ya kukipiga na
watoto wa Jangwani.
Baada ya kufanya mazoezi kwa siku nne mfululizo chini ya makocha Wabrazil Marcio Maximo, Leonardo Neiva na makocha wazawa Salvatory Edward, Shadrack Nsajigwa kwa pamoja wameridhiswa na uwezo wake na kuomba apewe kandarasi la kuitumikia klabu hiyo.
Emerson aliyekua akichezea katika timu ya Bonsucesso iliyopo daraja la pili kwenye jimbo la Rio de Janeiro alisaini mkataba huyo mbele ya Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto na anachukua nafasi ya mshambuliaji Geilson Santos Santana ‘Jaja’ ambaye ameshindwa kurejea nchini kutokana na matatizo ya kifamilia na kuomba klabu hiyo imuache.
Kocha Mkuu wa Yanga, Maximo amesema kuwa wameridhishwa na uwezo na kiungo mkabaji Emerson ana anaamini ataisaidia timu katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Kimataifa.
Yanga ni mwakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.
Ujio wa Emerson unafanya klabu ya Yanga kufikisha jumla ya wachezaji watano wa kimataifa, wengine wakiwa ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hamis Kizza na Andrey Coutinho.

0 maoni:
Post a Comment