Kama ilivyotarajiwa, ujio wa mshambuliaji Dan Sserunkuma Simba SC,
umekuwa na machungu kwa mshmbuliaji Mkenya Paul Kiongera ambaye uongozi
umeamua kumwondoa kikosini ili nafasi yake ichukuliwe na straika huyo
hatari wa timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’.
Wakati taarifa za awali kutoka ndani ya uongozi wa Klabu ya Simba zikidai wamemalizana na Sserunkuma, imefahamika kuwa Mganda huyo atatua tena nchini Jumatano kwa ajili ya kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo ya Msimbazi.
Aidha, Kiongera anatarajiwa kuondoka jijini Dar es Salaam kesho kwenda India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa goti, lakini klabu yake hiyo imemuondoa kwenye orodha ya wachezaji watakaocheza sehemu iliyobaki ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu ili kumwachia nafasi Sserunkuma.
Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia Patrick Phiri ameuambia mtandao huu jijini Dar es Salaam leo kuwa wamelazimika kuchukua hatua ya kumuondoa Kiongera katika kikosi chao ili wamsajili Sserunkuma kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.
“Jumatano Sserukuma atakuja tena Tanzania kwa ajili ya kumalizana na uongozi. Nimeambiwa mambo yalienda vizuri katika mazungumzo yao alipokuja Dar es Salaam wiki iliyopita,” Phiri amesema.
“Kiongera anakwenda India kutibiwa kesho, hivyo tumelazimika kumuondoa katika orodha ya wachezaji wetu msimu huu ingawa ataendelea kulipwa na Simba kulingana na matakwa ya kimkataba.”
Kiongera atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi miwili baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti lake alilojitonesha baada ya kugongana na kipa Shaban Kado wa Coastal Union dakika ya 88 ya mechi yao ya kwanza ya VPL msimu huu iliyomalizika kwa sare ya mabao mawili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Septemba 21.
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba zinaeleza kuwa wachezaji wengine kutoka nchi za Magharibi mwa Afrika wanakuja kufanya majaribio Simba na wakifuzu, kuna hatari ya wachezaji wa kigeni waliopo sasa akiwamo mfungaji bora wa VPL msimu uliopita, Mrundi Amissi Tambwe, watatemwa kwa vile wanadaiwa kushuka kiwango.
Mbali na Kiongera na Tambwe, wachezaji wengine wa kigeni wageni ndani ya Kikosi cha Simba ni Waganda beki Joseph Owino na mshambuliaji Emmanuel Okwi na kiungo Mrundi Pierre Kwizera.
Chanzo chetu ndani ya klabu hiyo kimeeleza kuwa mkataba wa Kiongera utasogezwa mbele kwa maana ya kipindi cha matibabu kutohesabiwa kama alikuwa kazini ingawa klabu itagharamia matatibu.
Kabla ya kuumia, Kiongera, anayedaiwa kuwa na matatizo ya goti tangu akiwa na mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, Gor Mahia, alicheza mechi tatu za kirafiki na kufunga mabao mawili kwenye kikosi cha Phiri cha Simba.

0 maoni:
Post a Comment