Awali wakati wa majira ya usajili nchini, timu ya kandanda ya Simba
SC iliamua kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake. Ikiwa chini
ya rais, Evance Aveva, Simba iliamua kumfuta kazi aliyekuwa kocha mkuu
wa timu hiyo, Mcroatia, Logarusic na kumuajiri, Patrick Phiri kutoka
Zambia. Mabadiliko yalifanyika hasa, wachezaji wa kila aina walisajiliwa
huku wale walioshindwa kufanya vizuri msimu uliopita wakiachwa.
Lengo ya uongozi mpya ilikuwa ni kuifanya klabu kurudi katika hali
yake ya ushindani ambayo katika kipindi cha miezi 34 sasa imeshuka kwa
kiwango kikubwa. Sijui sana kuhusu mwanzo wa tawala nyingine katika timu
hiyo ulivyokuwa, lakini katika kipindi cha 14 ya karibuni nadiriki
kusema, uongozi wa sasa umeanza vibaya zaidi. Sababu ni nyingi lakini
kubwa zaidi ipo katika utawala.
Sehemu ya wachezaji wa kikosi cha Simba SC kilichomaliza katika nafasi ya nne msimu wa 2013/14 katika ligi kuu Tanzania Bara.
Simba inayumbishwa na viongozi wake wenyewe ambao wanakataa kukubali
makosa waliyofanya mara baada ya kuingia madarakani. Kitendo cha
kuwafuta uanachama baadhi ya waliokuwa wanachama wa klabu kinawagharimu
wakati huu. Ulikuwa ni uamuzi ‘ mbaya’ ambao awali nilisema utakuwa
tatizo kwa timu. Hapa sizungumzii kuhusu sera za Aveva ambazo zilimfanya
aingie madarakani, kwani kama utazama na kugusa huko vile ilivyo sasa ‘
ameshindwa vibaya’, alikuwa na sera mbovu, lakini si hivyo ‘ sera ya
pointi 3’ imekufa, hivyo ni lazima zitazamwe sababu zilizofanya sera
hiyo kutokuwa na mafanikio.
Katika mchezo wa kwanza wa msimu huu, Simba ilicheza na Coastal Union
ya Tanga katika uwanja wa Taifa, ilionekana kama vile mambo yatakwenda
sawa msimu huu baada ya Shaaban Kisiga kufunga bao la ‘ mkwaju wa
penalti’. Lilikuwa bao la kwanza la msimu kwa Simba, na lilifungwa na
mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kikosini tena ‘ kwa kutumia maarifa
binafsi’. Amis Tambwe akafunga bao la pili, lakini mambo yalikuwa magumu
dakika 25 za mwisho. Coastal walichomoa mabao yote na kutengeneza sare
ya kufungana mabsao 2-2. Halikuwa tatizo, hakukuwa na hujuma.
Kiungo wa Simba SC aliyesimasimshwa Amri Kiemba ( kulia) akiwajibika
katika mchezo dhidi ya Polisi Morogoro ambao ulimalizika kwa sare ya
kufungana bao 1-1.
Mchezo wa pili ulikuwa ni dhidi ya Polisi Morogoro, pia ulipigwa
katika uwanja wa Taifa. Simba iliongoza kwa bao la mshambulizi, Emmanuel
Okwi. Ndani ya nusu saa ya mchezo. Mshambulizi wa zamani wa Simba
Danny Mrwanda akiitumia vizuri ‘ pasi ya kupenya’ iliyopigwa na kiungo
Salum Machaku na kuisawzishia timu yake dakika tano tu mara baada ya
kuanza kwa kipindi cha pili. Mechi ikamalizika kwa sarte ya kufungana
bao 1-1. Hapa kidogo maswali yakaanza kujitokeza, kiwango kibovu kutoka
kwa baadhi ya wachezaji kilifanya wengi kuanza kujiuliza kulikoni.
Amis Tambwe, mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania Bara, 2013/14 ambaye
tsayari amefunga bao moja msimu huu. Tambwe alifunga mabao 19 katika
michezo 24 msimu uliopita
UONGOZI, BENCHI LA UFUNDI, WACHEZAJI WAKAA KIKAO NA MATIZO YATAJWA….
Katika hali ya kutojiamini, ama kutoheshimu timu pinzani. Uongozi wa
Simba ulikaa chini na kufikia mwafaka wa kuhitisha kikao cha siri kati
ya utawala, benchi la ufundi na wachezaji. Bila uoga baadhi ya wachezaji
walisema kuwa matokeo ya sare mbili mfululizo yaliletwa na ushirikiano
mdogo uliopo katika timu. Hawakugusia mambo yaliyopo katika uongozi bali
walisema ‘ wachezaji kwa wachezaji’ hawapeani ushirikiano ule wa
kimpira wakiwa uwanjani. Ilikuwa no hoja ambayo ndani yake ina mantiki
kwa sababu kuna baadhi ya viongozi wameonekana kuwagawa baadhi ya
wachezaji na kuwapendelea wengine kwa sababu tu mchezaji Fulani
hajasajili na ‘ mtu/wati fulani’
Baada ya kikao hicho mambo yalikwenda vilevile. Mchezo wa tatu
ulikuwa ni dhidi ya Stand United ya Shinyanga ambao nao ulifanyika
katika uwanja wa Taifa. Kisiga akitokea benchi kuchukua nafasi ya Said
Ndemla aliyeumia alifunga bao lake la pili msimu huu, pia lilikuwa bao
la kwaju ‘ uliokufa’. Katika ligi ambayo mabao kadhaa yamefungwa kwa
mipira ya adhabu ndogo, Kisiga angweza kuipa Simba pointi ‘ tatu za
kwanza’ msimu huu kama tu safu ya ulinzi isingeendeleza ‘ tabia yao ya
kukubali kuruhusu bao la kuswazishwa’. Mwishoni mwa mchezo Stand
walichomoa na kutengeneza sare ya ‘ Tatu mfululizo katika uwanja wa
nyumbani’.
Haroun Chanongo naye pia amesimamishwa
Katika mchezo wowote huwa tunasema; ‘ asiyekubali kushindwa, si
mshindani’, lakini katika fikra za kishabiki, matokeo ya Simba
yalipangwa. Hivyo ndivyo wanavyoamini baadhi ya viongozi. Nahodha,
Joseph Owino aliwekwa benchi katika mchezo dhidi ya Stand na nafasi yake
kuchezwa na chipukizi, Joram Mvegeke. Sijui kama yalikuwa ni
mapendekezo ya Phiri mwenyewe kama mkuu wa benchi la ufundi, au ni
muendelezo wa makocha ‘ dhaifu wa kigeni’ ambao wanaendeshwa ‘ kwa
rimoti’ na baadhi ya watu wenye kuwashikilia?. Kama tatizo la kwanza
ilionekana ni Owino, Simba hawakung’amua chanzo cha tatizo lenyewe.
Je, baada ya Owino kuwekwa benchi, safu ya ulinzi ilifanya kazi nzuri
zaidi?. Matokeo yalikuwa ni ‘ yale yale tu’. Mchezaji pekee ambaye
hajakosekana katika safu ya ulinzi ya Simba msimu huu ni Hassan Isihaka.
Kiwango chake ni kizuri lakini kama sababu ni hujuma, wengine wote
waliofanyiwa mabadiliko hawakuleta afadhali yoyote hadi pale Owino
alirudishwa katika mchezo dhidi ya Yanga ambao ni pekee Simba
hawakufunga bao wala kuruhusu goli msimu huu.
Kihistoria, Simba ilipaswa kuchukua pointi tatu dhidi ya Polisi Moro
kwa sababu huwa hawana uwezo wa kuifunga timu hiyo ya Morogoro ikiwa
nyumbani katika miaka ya karibuni. Sare dhidi ya Coastal ni kielelezo
cha ugumu wa ligi ya msimu huu, sare ya Stand ni matokeo ya soka tu.
Huku suluhu dhidi ya Yanga ilichukuliwa kama ‘ mwisho wa matatizo’.
Hawakujua, kumbe ni mwanzo wa kuelekea kipigo cha kwanza msimu huu.
KUWATIMUA KAMBINI, KIEMBA, KISIGA NA CHANONGO………
Wakati Fulani msimu uliopita ulipokuwa ukielekea mwishoni, niliwahi
kuhoji kiwango cha kiungo Haroun Chanongo. Ukweli wakati ule wa mchezo
dhidi ya Mbeya City uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 niliamini
kuwa, Chanongo ni mchezaji mwenye ‘ tabia ya kupanda na kushuka kwa
kiwango chake’. Lakini kuanzia msimu huu, mchezaji huyo amekuwa juu,
lakini ametimuliwa kambini kwa sababu za kudaiwa kuchangia matokeo
mabaya ya timu. Kivipi?
Okwi alifunga bao la kuongoza kwa timu yake na kuifanya iwe mbele kwa
bao 1-0 katika uwanja ambao wameishinda, Tanzania Prisons mara mbili tu
katika kipindi cha miaka 14 sasa. Zikiwa zimesalia tano mchezo
kumalizika Prisons waliswazisha. Simba imepata pointi ya kwanza katika
uwanja wa ugenini msimu huu baada ya kufungana bao 1-1 na Prisons lakini
hilo limeambatana na kusimamishwa kwa baadhi ya wachezaji. Chanongo,
Kiemba na Kisiga. Lakini katika hali ya kimpira tuhuma hizo si za kweli
zaidi ya ‘ chuki binafsi alizonazo’ mwenyekiti wa kamati ya usajili kwa
wachezaji hao ambao hakuwasajili yeye. Majuzi alisikia mwenyekiti huyo
wa kamati ya usajili akisema kuwa kila anapopangwa Kiemba timu yao
haishindi. Je, huu ndiyo weledi wa kiuongozi. Ule mgawanyiko ambao
wachezaji waliusema katika kikao unaletwa na viongozi kama hawa ambao
wanasema tu wachojisikia.
Nathubutu kusema kuwa baada ya sare tano mfululizo, Simba itapigwa na
Mtibwa Sugar wikiendi ijayo na baada ya hapo atakayefuata ni kocha
Patrick Phiri. Lakini Simba SC inaharibiwa na hao jamaa zao wenyewe, ‘
Watu wakubwa’. Wakati wa uongozi wa Mh. Aden Rage nilikuwa nikipenda
kutumia sentesi ya ‘ Mtu mkubwa ni Mwanafunzi’, hutamani vitu vingi
zaidi. Labda Phiri apange wachezaji wote waliosajiliwa na ‘ Mbwana
Mkubwa’ ndipo Simba itashinda!!. Nyakati za furaha zimepotea klabuni
huku ndani ya uwanja matokeo yakiwa ‘ hovyo’.
Felix Sunzu ( kushoto) marehemu, Patrick Mafisango ( katikati), na
Emmanuel Okwi wakishangilia moja ya ushindi wa Simba msimu wa 2011/12
ambao Simba ilitwaa ubingwa wa mwisho.
Msiwape lawama ‘ wale-Simba Ukawa’ ambao hawajulikani wanaishi wapi,
‘ adui wa kwanza wa Simba ni Pesa’, Si Kiemba, Kisiga wala Chanongo.
Niliwahi kuandika ‘ Phiri atafukuzwa kazi Simba SC…..’, Phiri yupo
katika ‘ shinikizo la chinichini’ hivi sasa. Hakuna, Simba ukawa ila
kuna watu ndani ya Simba yenyewe wanataka Simba ifungwe sasa na si kutoa
sare, unajua ni kwa nini? Mtu mkubwa ni Mwanafunzi tu.