KUELEKEA NGAO YA JAMII, YANGA YAENDELEA KUJIFUA

Hamis Kiiza (kushoto), Kelvin Yondani (katikati) na Mrisho Ngassa (kulia) wakiwa mazoezni leo asubuhi kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam FC jumamosi
Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Young Africans kimeendelea na mazoezi katika viwanja vya shule ya sekondari Loyola kujiaanda na mchezo wa Ngao ya Hisani siku ya jumamosi  Agosti 17, 2013 dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans wanakutana na Azam FC katika mchezo ambao Yanga wanahitaji kuendeleza wimbi la ushindi kufuatia kuwa imeshinda michezo yake mitatu mfululizo dhidi ya wana lamba lamba Azam FC kwa msimu uliopita.
Kocha mkuu Brandts ameendelea kuwanoa vijana wake kuhakikisha wanaedelea kuwa fit kiakili, kimwili na kiafya na morali waliyonayo waendelea kuwa katika kiwango cha juu na kupata ushindi katika michezo inayokuja.
Wachezaji wote wamefanya mazoezi leo na habari njema ni kurejea kwa mshambuliaji wake Hamis Kiiza aliyekuwa nchini Uganda kwa kambi ya timu ya Taifa kabla ya jana kuja kunganana wenzake kuiandaa na mchezo huo.
Katika michezo mitatu iliyopita Yanga dhidi ya Azam FC, watoto wa Jangwani wameshinda michezo yote mitatu, mchezo wa kwanza fainali ya Kagame 2-0, mzunguko wa kwanza 2-0 na mzunguko wa pili 1-0 sawa na
P3 W3 D0 L0 GF5 GD 0 PTS9.
Wachezaji waliofanya mazoezi leo ni:
walinda mlango: Ally Mustapha 'Barthez', Deogratius Munishi 'Dida; na Issa Kazembe
Walinzi wa pembeni: Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua na David Luhende
Walinzi wa kati : Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani 'Cotton', Rajab Zahir, Ibrahim Job
Viungo: Salum Telela, Athuman Idd 'Chuji', Frank Domayo, Nizar Khalfani, Hamis Thabit, Bakari Masoud
Washambuliaji wa Pembeni: Mrisho Ngassa, Saimon Msuva, Abdallah Mguhi 'Messi'
Washambuliaji wa kati: Said Bahanuzi, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Shaban Kondo, Hussein Javu na Jerson Tegete 

0 maoni:

Post a Comment

 
Top