Home
»
»Unlabelled
» SHILOLE ASHUSHIWA KIPIGO KISA MADENI...!!
Msanii nyota kwenye tasinia ya muziki na filamu bongo Zuwena Mohamed “ Shilole” mwishoni mwa wiki iliyopita alionja joto ya jiwe baada ya kutiwa mtu kati na wakina dada waliokuwa wanamdai kiasi kikubwa cha pesa.
“ Ishu ilikuwa hivi sisi tunamdai huyu dada lakini cha kushangaza amekuwa akitupiga chenga sana na ona alivyokuwa sio mstaarabu kumbe siku hiyo alikuwa anahama na deni letu ndio maana tuliamua kwenda kumzingua” Alisema dada huyo aliomba jina lake lihifadhiwe.
“ Unajua sisi tunafanya biashara zetu hivyo kuna siku Shillole alikuja na kusema amekwama kipesa hivyo tumuazime pesa na tukafanya hivyo lakini cha kushangaza mwezi wa sita huu hataki kurudisha na amekuwa akitukwepa mara kwa mara hivyo majirani ndio wakatushtua kuwa anataka kuhama kwa staili ya kutoroka na deni letu ndipo tulipoenda wanawake wanne na kumshushia kipigo” Alisema dada huyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 maoni:
Post a Comment