Hatimaye sakata la usajili la mchezaji Gareth Bale wa Tottenham Hotspur limefikia mwisho baada ya mchezaji huyo kujiunga na klabu ya Real Madrid.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka kwenye mtandao wa Spurs ni kwamba klabu hiyo imefikia makubaliano na klabu ya Real Madrid kuhusu usajili wa Bale.
Gareth Bale alijiunga na Spurs akitokea Southampton mnamo mwaka 2007, ameichezea Spura mechi 203 na kufunga mabao 55.
Mpaka sasa vilabu vyote vimethibitisha usajili wa Bale lakini hakuna ambayo ametoa gharama halisi za usajili huo, vyanzo tofauti vikiripoti kuwa ni £86m japo hakuna uthibitisho rasmi.
Bale atasaini mkataba wa miaka 6 wa kuitumikia Real Madrid
0 maoni:
Post a Comment