Jitihada za kurejesha heshima kwa viwanja vya ndege nchini zilizoanzishwa na waziri wa uchukuzu Dk. Harisson Mwakyembe zinaonekana kuzaa matunda baada ya mwanadada kutoka nchini Nigeria Anthonia Ojo (25) kukamatwa na kete 99 za madawa ya kulevya dar es salaam jana.
Mwanamke huyo amekamatwa akieleke Roma Italia kupitia Paris Ufaransa kwa ndege ya Ethiopian Airways na aliingia hapa nchini Agosti 30 akitokea Nigeria.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Viwanja vya Ndege, Renatus Chalya, Ojo ataendelea kubaki chini ya ulinzi wa polisi kwa uchunguzi zaidi, wakati madawa hayo yamepelekwa kwenye ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini aina ya dawa hizo na thamani yake...
0 maoni:
Post a Comment