Uhamisho wa beki Eliaqum Mangala na mwenzie Fernando kutoka umekwamba na wachezaji hao wameonekana kwenye ndege wakielekea jijini Madeira kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Ureno kesho.
Papiss Cisse amekataa kujiunga na klabu ya Uturuki Trabzonspor lakini msenegal huyo bado anaweza kuuzwa usiku huu ikipatikana ofa ambayo Newcastle wanaitaka.
Borussia Monchengladbach bado wanamhitaji mshambuliaji wa Newcastle.
Wilfred Zaha amejiunga rasmi na Cardiff City kwa mkopo akitokea Manchester United |
Chelsea wamethibitisha kumsajili Kurt Zouma kutoka St Etienne, lakini mlinzi huyo ataendelea kubakia kwenye timu hiyo ya Ufaransa mpaka mwisho mwa msimu.
Kinda hilo lenye miaka 19 amejiunga na Chelsea kwa mkataba wa miaka mitano na nusu.
Emmanuel Frimpong amejiunga na Barnsley akitokea Arsenal |
Kocha wa Manchester United amethibitisha rasmi kwamba wapenzi wa klabu hiyo wasitegemee kusajiliwa kwa mchezaji yoyote leo hii zaidi baadhi ya wachezaji wataondoka kwa mkopo.
Adel Taarabt amekamilisha usajili wake wa kujiunga na AC Milan akitokea QPR |
Lewis Holtby amekamilisha uhamisho wake kutoka Tottenham kwenda Fulham kwa mkopo |