Barcelona wamekanusha madai kwamba wamempa mkataba mpya golikipa Victor Valdes.
Msimu uliopita golikipa huyo wa kihispania alitangaza uamuzi wake wa kuondoka Camp Nou wakati mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa msimu huu.
Lakini Radio Marca ilisema kwamba mabingwa watetezi wa la liga wamejaribu kubadili uamuzi wa kipa huyo mwenye miaka 32 kwa mara ya mwisho.
Taarifa kutoka Barca ilisema: "FC Barcelona inakanusha taarifa iliyotolewa jioni(jana) na radio Marca kuhusu ofa ya mkataba mpya wa Victor Valdes.
“Klabu inaheshimu uamuzi wa mchezaji. Tungependa kuonyesha shukrani, ueledi kwenye suala hili."
Barcelona bado wamekuwa wakihusishwa na magolikipa kadhaa kama wabadala wa Valdes, akiwemo golikipa wa Borussia Monchengladbach Marc Andre ter Stegen.