Mwamuzi msaidizi Scott Ledger jana usiku alikuwa na mchango mkubwa kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu nchini England baada ya kutoa maamuzi tata yaliyoisaidia Manchester City kuifunga Totenham mabao 5-1.
Kwenye mchezo huo mwamuzi huyo aliipa Man City penati ambayo haikustahili kutokana na beki wa Spurs Danny Rose kuucheza mpira kwanza kabla ya mshambuliaji Edin Dzeko hajaanguka chini.

Maamuzi hayo yalipelekea beki huyo kupewa kadi nyekundu ikiwa ni pamoja na adhabu ya penati ilikwamishwa wavuni na Yaya Toure.





 
Top