torres_pa_2715315b
Chelsea wanaelekea kwenye uwanja wa Etihad usiku wa leo kukutana na timu inayopewa nafasi kubwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England Manchester City. City kwa sasa wanatisha na rekodi yao nzuri kwa asilimia 100 katika uwanja wao wa nyumbani wakiwa wamefunga mabao 42 katika michezo 11 tu nyumbani kwao, kwa wastani wa mabao 3.8 kila mechi. 

 Chelsea inawapasa kuwa na wasiwasi kwa sababu City tayari wameshaweka kambani mara 6 katika mchezo dhidi ya Spurs na Arsenal, huu wakimtandika Moyes 4. Kwa maana hiyo kutokana na uwezo mkubwa wa City katika kushambulia je mbinu nzuri kwa Chelsea leo ni kucheza kwa counter-attack Chelsea?

Jose Mourinho ataipanga vipi timu yake? 
Jose Mourinho aliwasema sana West Ham kwa mchezo wao aliouita "Soka la 19th century’ baada ya vijana wa Sam Alladyce kupaki basi golini katika mchezo wao wa Jumatano iliyopita, Mourinho alikasirishwa na namna West Ham walivyokuwa wakizuia, kukaa nyuma ya mpira, na kuzidi kuchanganywa zaidi kuona timu yake ikikosa mbinu za kuipasua ngome hiyo.

Uchezaji wa aina hii wa soka sio mgeni hata kidogo kwa Mourinho ambaye amekuwa akiitumia staili hii kwa miaka yote ya ufundishaji wake. Kwa Chelsea itakuwa tofauti na West ham. Chelsea wanaweza kujipanga kwa mfumo wa  4-3-3/4-5-1, kama vile walivyocheza pale Emirates mwishoni mwa 2013 ambapo waliweza kuzuia Arsenal kutengeneza nafasi.

Utatu mtakatifu wa viungo Nemanja Matic, Ramires na Frank Lampard unaweza kufaa kabisa kwenye mchezo huu, huu Hazard na Willian wakicheza pembeni kufanikisha mashambulizi ya kushtukiza. City watajaribu kucheza 4-4-2, wakicheza na viungo wawili tu wa kati. Fernandinho na Yaya Toure ambao wote wana nguvu lakini kwa utatu wa viungo wa Chelsea wanaweza kuwapunguza kasi na kuleta madhara kwao Cech. Matic ambaye ana kimo cha 6’4 anaweza kuwa mtu muhimu baada a kuonyesha kiwango kizuri hasa katika mchezo dhidi ya timu ngumu ya Stoke City.

Huku Willian akicheza kwenye shavu la kulia, Chelsea watakuwa na mchezaji ambaye anaweza kurudi na kuzia vizuri kuliko wachezaji wa ushambuliaji, lakini ana uwezo mzuri wa kukimbia na kushambulia wakati wa counte attacks. Hazard anaweza kuchukua mpira nyuma na kuanzisha mashambulizi, akiwa tayari ametimiza 81 dribbles msimu huu, idadi kubwa kuliko mchezaji yoyote kwenye premier league.

Ikiwa Chelsea watazuia vizuri watayafanya maisha kuwa magumu ka City, na wanaweza kuwa timu ya kwanza kupata matokeo chanya Etihad baada ya muda mrefu. Rekodi ya kuzuia ya Chelsea ndio bora kabisa kwenye ligi, wakiwa na clean sheets tano katika mechi 7 zilizopita za ligi.

Hitimisho

Kuwachezesha Hazard na Willian kwenye winga kunaweza kuiletea matatizo City katika counter attacks. Ikiwa Chelsea wataendelea kucheza kupitia mfumo wa 4-2-3-1, watakuwa wanajiweka pabaya mbele ya walafi wa kufunga mabao City, wakimtumia David Silva kuingia ndani akitoka winga na kuja kuongeza mtu katika eneo la kati ya kiungo cha Chelsea na eneo la ulinzi.  Chelsea ni underdogs kwenye mchezo huu, lakini vizuri kukumbuka Arsenal waliweza kufunga mabao matatu kwenye mechi yao dhidi ya City, na hilo linaonyesha namna kikosi cha Manuel Pellegrini kilivyo na nyufa kwenye ulinzi.
 
Top