Washindi: Adam Nditi mbele ya bango kulia akiwa na wachezaji wa Chelsea wakisherehekea taji lao la U-21 la ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kuifunga Manchester United mabao 2-1 katika fainali jana Uwanja wa Old Trafford
 
MTANZANIA Adam Nditi jana alicheza kwa dakika zote 90 wakati Chelsea ikiichapa Manchester United mabao 2-1 na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 21 England Uwanja wa Old Trafford. 
 
Nditi na mchezaji mwenake wa Chelsea, Swift walionyeshwa kadi za njano katika mcheo huo uliohudhuriwa na kocha wa muda wa United, Ryan Giggs na msaidizi wake, Paul Scholes sawa na Pearson na Ekangamene kwa upande wa Mashetani Wekundu.
Mtanzania Ulaya: Kiungo Adam Nditi wa Chelsea kushoto akimkabili Varela wa Man United na kulia na mchezaji mwenzake, Nathan Ake.
Katika mechi hiyo tamu ya fainali, United walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 12 kupitia kwa Lawrence, kabla ya Charly Musonda kuisawazishia The Blues dakika ya 21 na Lewis Baker kufunga la ushindi dakika ya 78.
 
Top