Luke Shaw amekamilisha dili la usajili la paundi milioni 31.5 katika klabu ya Manchester United
BEKI wa kushoto wa England, Luke Shaw amekamilisha usajili katika klabu ya Manchester United kwa dau la paundi milioni 31.5 na kusaini mkataba wa miaka minne kukipiga Old Trafford.
Nyota huyo kinda amefuzu vipimo vya afya leo katika uwanja wa mazoezi wa Carrington na imetaarifiwa kuwa atakuwa chaguo la kwanza la kocha Louis van Gaal katika nafasi ya kushoto.
Inafahamika kuwa kinda huyo atahakikishiwa nafasi ya kuanza, huku beki mkongwe mwenye miaka 33, Mfaransa, Patrice Evra ambaye atabakia kwa mwaka mmoja akipunguziwa majukumu.
Historia: Shaw alisema amejisikia furaha kujiunga na mabingwa mara 13 wa ligi kuu ya Englang.