article-2671432-1F2AF91B00000578-334_634x425
HATUA ya Makundi ya kombe la dunia linaloendelea kushika kasi nchini Brazil imekamilika jana na kushuhudia timu mbili za Afrika zikitinga hatua ya 16.
Sare ya bao 1-1 baina ya Algeria dhidi ya Urusi imewafanya wanaume hao wa Afrika kufuzu hatua ya mtoano, lakini Nigeria walikuwa wa kwanza kufuzu licha ya kufungwa mechi ya mwisho mabao 3-2 dhidi Argentina.
Timu za Cameroon, Ivory Coast, na Ghana zimeshafungasha virago.
Ratiba ya mtoano itashuhudia timu za Afrika zikivaana na mabingwa wa zamani wa michuano hiyo mikubwa katika ulimwengu wa soka.
Nigeria maarufu kama Super Eagles watachuana na Ufaransa ya akina Karim Benzema.
Algeria watakuwa na kibarua kikali dhidi ya Ujerumani ya Thomas Muller.
Mechi nyingine zitawakutanisha wenyeji Brazil dhidi ya Chile, Colombia dhidi ya Uruguay, Uholanzi na Mexico, Argentina na Uswisi, Ubelgiji wao watachuana na Marekani.
 
Top