Mabingwa wa kandanda Tanzania Bara, klabu ya Azam FC wameingia katika wiki ya tatu ya maandalizi ya msimu mpya wa 2014/15 ambao unataraji kuanza katikati ya mwezi ujao. Azam ilianza mazoezi wiki mbili zilizopita chini ya Walimu wasaidizi, Kally Ongala na Ibrahimu Shakanda, kabla ya kocha mkuu, Patrick Omog kujumuika na wachezaji wa kigeni mwanzoni mwa wiki iliyopita.
Azam ilifanya maboresho katika kikosi kwa kuwasaini wachezaji, Didier Kavumbagu na Frank Domayo ambao walikuwa huru baada ya kumaliza mikataba yao na klabu ya Yanga. ‘ Kavu’ alifunga mabao 11 msimu uliopita ikiwa ni mara yake ya pili kufunga idadi hiyo ya mabao katika msimu mmoja. Msimu wake wa kwanza katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mshambulizi huyo raia wa Burundi, alifunga mabao 11 na kushinda ubingwa wa ligi kuu akiwa na Yanga SC.
Usajili huu si kamari kwa Azam na hata kwa Kavumbagu mwenyewe. Kufunga mabao 22 katika misimu miwili hilo si jambo dogo. Katika ligi ambayo washambuliaji wa kigeni wameshindwa kutamba ndani ya uwanja. Yanga wanaweza kujutia uamuzi wa kumuacha aondoke, mbaya zaidi ameondoka kama mchezaji. Kavu ametoa mchango mkubwa kwa Yanga katika muda wa miaka miwili aliyokuwa mchezaji wa timu hiyo, Yanga pia wamepata faidi kutoka kwa mchezaji huyo kwani amewapatia ubingwa na mabao yake msimu uliopita yameweza kuisaidia timu hiyo kupata nafasi ya kuiwakilisha nchini katika michuano ya kombe la shirikisho Afrika, Mwaka ujao.
Kwa upande mwingine, Yanga hawatajuta kwa kumuacha, Kavumbagu aonde kama mchezaji huru kwa kuwa tayari wamepata matunda kutoka kwa mchezaji huyo.
Ukiachana na uwezo wake wa kufunga mabao, mchezaji huyo ni mtu anayewajibika vilivyo katika mkaba wake. Alikuwa mtulivu na asiye na safari za mara za mara kwenda kwao, na pale ilipotokea alikuwa akirejea kwa wakati mwafaka klabuni. Mfungaji hatari wa mipira ya kichwa, na mshambulizi mwenye umakini ndani ya eneo la hatari. Pengine kucheza sambamba na John Bocco, Kipre Tcheche, Brian Omony katika timu moja kunaweza kumfanya kuongezea umakini zaidi kila anapopata nafasi ya kucheza.
Azam haijabahatisha katika kumsaini, Kavu, walifunga mabao 51 katika michezo 26 msimu uliopita, walizidiwa mabao kumi na timu iliyomaliza katika nafasi ya pili. Lakini kitendo cha kumsaini mshambulizi huyo aliyefunga mabao 11 katika ya 61 ya Yanga msimu uliopita. Kipre Chetche amefunga jumla ya mabao 31 katika misimu miwili katika ligi kuu ya Bara. Kipre, mchezaji bora wa msimu uliopita alikuwa kinara wa mabao kwa timu yake baada ya kufanikiwa kufunga mabao 14. Alimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Amis Tambwe wa Simba SC katika tuzo ya mfungaji bora. Lakini mfungaji huyo bora wa msimu wa 2012/13 aliteremka kwa mabao matatu , kwani alichukua tuzo ya ufungaji bora mwaka jana akiwa na mabao 17.
Kama, Kavumbagu atatulia katika timu hiyo mabao yake 11 kwa msimu yatatosha kwa timu yake, kwa kuwa hakuna mchezaji mwingine yeyote alimudu kufunga mabaop kuanzia kumi katika msimu uliopita. Alipowasili kocha Omog haraka alisema kuwa timu hiyo inahitaji mabadilko makubwa ya wachezaji. Baada ya kuona viwango vya chini kutoka kwa wachezaji, mwalimu huyo raia wa Cameroon aliwekeza zaidi mbinu zake kwa wachezaji tofauti kikosini huku kila mchezaji ndani ya uwanja akiwajibika kufunga mabao kadri inavyowezekana.
Mtindo huo wa kichezaji uliibeba sana Azam hasa katika michezo ambayo ilitoa taswira za ugumu kwa upande wao. Timu ilimaliza msimu bila kupoteza mchezo wowote, walikusanya pointi 14 kwa timu za Yanga, Mbeya City na Simba ambazo zilimaliza katika nafasi nne za juu. Kipre alifunga kwa kila timu katika michezo hii, hivyo inaonesha wazi kuwa kocha Omog anatafuta mtu wa kumsaidia katika jukumu hilo. Nahodha, Bocco amekuwa mchezaji wa majeraha ya mara kwa mara kwa misimu miwili sasa.
Bocco, mfungaji bora wa ligi kuu msimu wa 2011/12 alifunga mabao kila alipikuwa fiti na aliendelea kuwa mchezaji wa mechi kubwa kila alipohitajika. Alifunga katika kila mchezo dhidi ya Simba msimu uliopita. Alifunga bao moja katika ushindi wa Azam wa mabao 3-2 dhidi ya Yanga na alifunga bao ambalo liliwapa taji la kwanza dhidi ya City katika uwanja wa Sokoine, Mbeya wakati Azam ilipoicha Mbeya City mabao 2-1. Bocco alifunga mabao sita tu msimu uliopita. Hivyo kama safu ya ulinzi isingekuwa imara mambo yangekuwa mabaya kwa timu.
Kusajiliwa kwa Kavumbagu kumeongeza machaguo katika safu ya mashambulizi, ukitoa washambuliaji hao wane, Gaudensi Mwaikimba Hamis Mcha wataongeza ushindani na ubadilikaji wa fomesheni kwa timu kulingana na wachezaji wanavyokuwa wakiwajibika. Azam ni timu ambayo imetulia hivyo wachezaji wamekuwa wakitumia utulivu huo kuishi kama familia moja inayohitaji mafanikio. Kusajiliwa kwa Kavumbagu kumeongeza idadi ya mabao klabuni, ushindani katika safu ya mashambulizi.
Bahati mbaya kwa Azam ni kutomtumia kiungo, Domayo katika michezo ya raundi ya kwanza kutokana na mchezaji huyo kuwa majeruhi. Wakati atakaporejea uwanjani, michuano ya kimataifa itakuwa usoni na mchezaji huyo anaweza kuongeza hamasa kikosini wakati ambao timu inawahitaji wachezaji bora kama yeye katika michuano ya kimataifa. Domayo amecheza vizuri katika michezo yote ya Yanga katika klabu bingwa Afrika, mapema mwaka huu. Amekuwa mchezaji wa timu ya Taifa kwa miaka miwili sasa hivyo sababu mojawapo ya kocha Omog kuwaamsha wachezaji ni kuwaletea washindani wa uhakika katika kila nafasi. Kwa sasa usajili huu ghali zaidi hasdi sasa katika majira haya ya usajili unaweza kuonekana ni hasara kwa kuwqa m,chezaji huyo amesajiliwa akiwa ni majeruhi, lakini ni faida ya muda mrefu kwa Azam na atatoa matunda kila atakapokakuwa akikanyaga uwaga.
Ismail Diarra bado hajaonekana machoni mwetu kwa maana kuwa hakuna ambayew anaweza kumjaji kwa lolote wakati huu akijiandaa na msimu wake wa kwanza katika ligi kuu. Makocha wengi hupenda kusajili wenyewe wachezaji katika vikosi vyao. Wakati mwingine huwa na sababu za kimpira na kuwa wengine hufanya hivyo kwa sababu za kimaslai. Kama, mwalimu aliyeshinda taji la Afrika kwa upande wa klabu, sina shaka na uamuzi wa Omog kumsaini, Diarra. Kiufundi makocha hupenda kiuwekeza mbinu zao kwa wachezaji maalumu na pengine huyu, raia wa Mali atatumiwa kama kiungo wa mawasiliano ndani ya uwanja kati ya kocha na wachezaji.
Ikumbukwe kuwa siku chache baada ya kushuhudia kikosi chake kikitupwa nje ya michuano ya kombe la Shirikishho na Ferreviario ya Msumbiji, kocha huyo alisema kuwa wachezaji wake hawakidhi viwango vya uwekezaji uliofanywa katika timu hiyo, alimaanisha kuwa mchezaji bora ndiye anayepaswa kuvaa jezi za Azam na kuiwakilisha katika mashindano. Hivyo sifikiri kama anaweza kumleta mchezaji wa hovyo katika timu hiyo.
Hadi sasa, Azam FC imefanya maboresho mazuri katika kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao na michuano ya kimataifa, wachezaji wa zamani wakubali changamoto mpya na kuwakaribisha vizuri kikosini wachezaji wapya ili wafurahi tena, Mei, Mwakani wakiwa na taji la ligi kuu. Azam imejiimarisha vizuri kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, na michuano ya klabu bingwa Afrika