Brazil-vs-Germany-2014-World-Cup-Semi-finals-Football-Wallpaper-1024x576
Uholanzi ilifuzu kwa mara ya pili mfululizo nusu fainali ya kombe la dunia baada ya kuwashinda timu ya Costa Rica kwa changamoto ya mikwaju ya penalti dhidi ya Costa Rica katika mchezo pekee wa robo fainali ambao ulichezwa kwa dakika 120 na matokeo kuwa suluhu-tasa.
Sasa ‘ wataalamu wa soka la mbinu’ Ujerumani na Uholanzi watakutana na timu zenye vipaji kutoka ‘ bara la soka’. Kwa mara ya kwanza timu za Brazil na Argentina zimefuzu kwa wakati mmoja hatua ya nusu fainali na mafanikio yametokana na timu hizo kucheza kwa ushirikiano na umakini mkubwa katika michezo mitano iliyopita.

 
Top