Timu hizo zimekutana mara nne katika iaka 11 iliyopita. Thiery Henrry, na David Trezeguet ambaye alifunga mabao mawili waliisaidia Ufaransa kuifunga Ujerumani kiwa mabao 3-0 novemba, 2003 katika mchezo wa kiimataifa wa kirafiki. Kipigo hicho ni kikubwa zaidi kwa Ujerumani kutoka kwa Ufaransa. Miaka miwili baadae Ufaransa ililazimisha suluhu-tasa katika uwanja wa nyumbani. Februari, 2012 Ufaransa iliifunga tena Ujerumani kwa mabao 2-1. Oliver Giroud na Florent Malouda walifunga mabao ya Ufaransa, wakati bao la kufutia machozi ya Ujerumani lilifungwa na Cacau katika dakika ya 90.
Ushindi pekee wa Ujerumani ni ule wa februari, 2013 waliposhinda kwa mabao 2-1. Kiungo Mathieu Valbuena alifunga bao la kuongoza kwa Ufaransa katika dakika ya 44, kabla ya Thomas Muller na Sam Khedira kufunga mabao mawili katika kipindi cha pili na kuisaidia Ujerumani kuibuka na ushindi huo. Makocha wote wamekutana tena baada ya miezi 16 na safari hii si katika michezo ya mtoano bali robo fainali ya kombe la dunia.
Timu hizo zimekutana mara moja katika mchezo wa kombe la dunia. Ufaransa iliifunga Ujerumani kwa mabao 6-2 huku mshambulizi wake, Fontaine akifunga mabao manne na kuweka rekodi ya kufunga mabao 13 katika fainali za mwaka 1958. Mchezo huo dhidi ya Ujerumani ulikuwa ni wa kusaka mshindi wa tatu. Mwaka 1982 Ufaransa ilifungwa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti katika mchezo wa nusu fainali. Mchezo huo unakumbukwa na wengi kwa kuwa ulitawaliwa na matukio mengi mabaya kutoka kwa wachezaji wa Ujerumani.
ROBO FAINALI YA 13 KWA UJERUMANI WAMEPOTEZA MARA NNE
Ujerumani imeshindwa mara nne tu kuvuka hatua ya robo fainali kati ya mara 12 walizofanikiwa kufika miaka ya nyuma, mara ya kwanza ni katika fainali za mwaka 1962 walipofungwa na iliyokuwa Yugoslavia kwa bao 1-0, wakashindwa kuvuka makundi ya timu nane bora katika fainali za mwaka 1978 zilizofanyika nchi Argentina na mara zote mbili za mwanzo walikwama katika fainali zilizofanyika barani Amerika Kusini. Waliishia tena robo fainali katika fainali za mwaka 1994 walipofungwa na Bulgaria kwa mabao 2-1. Fainali hizo zilifanyika nchini Marekani.
Kipigo chao kikubwa katika michuano hiyo kilitoka kwa Croatia katika robo fainali mwaka 1998 nchini Ufaransa ilipokubali kichapo cha mabao 3-0. Kuanzia hapo timu hiyo imecheza michezo 21 mfululizo ya fainali tatu zilizopita. Ilifungwa na Brazil katika mchezo wa fainali mwaka 2002 kwa mabao 2-0, walipoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Italia mwaka 2006 katika fainali zilizofanyika nyumbani kwao, na walianguka tena katika hatua ya nusu fainali mbele ya Hispania mwaka 2010. Mchezo wao dhidi ya Ufaransa sit u kuwa wa 104 katika michuano hiyo bali utakuwa ukifikia rekodi ya Brazil ambao walicheza michezo 26 mfululizo kuanzia mwaka 1994 hadi 2006. Ujerumani wamefikia rekodi hiyo.
UFARANSA BINGWA MARA MOJA vs BINGWA MARA TATU MWENYE FAINALI SABA
Ufaransa imefuzu mara 14 fainali za kombe la dunia. Ni moja ya timu tatu ambazo zimewahi kufuzu michuano hiyo mara sita mfululizo kuanzia iliposhiriki kwa mara ya kwanza katika fainali za mwaka 1930 nchini Uruguay. Chini ya wakali Raymond Kopa, Justine Fontaine ( ambaye anashikili rekodi ya kufunga mabao mengi katika fainali moja) Ufaransa ilifanikiwa kuchukua nafasi ya tatu katika fainali za mwaka 1958 nchini Sweden. Yalikuwa mafanikio yao ya kwanza ya juu katika michuano hiyo.
Ubingwa wao wa kwanza ni ule wa mwaka 1998 chini ya kizazi cha kina Zidane. Ujerumani imepoteza mchezo wa fainali mara nne. Ufaransa ilipoteza robo fainali ya kwanza mwaka 1938 walipochapwa na Italia kwa mabao 3-1 baada ya hapo hawajawahi kupoteza mchezo war obo fainali. Wamefanikiwa kuvuka hatua hiyo mara nne .
WACHEZAJI HATARI KWA TIMU ZOTE BRAZUCA 2014
Mshambulizi, Karimu Benzema alibanwa sana na walinzi wa Nigeria katika mchezo wa hatua ya 16 bora, lakini anaweza kuamka upya na kuendeleza kufunga mabao katika michuano inayoendelea. Benzema amefunga mabao manne katika michezo minne aliyocheza nchini Brazil. Ni sawa na Thomas Muller wa Ujerumani ambaye alibanwa pia katika mchezo wa 16 bora na Algeria naye amefunga mabao manne. Washambuliaji hawa wanaweza kuzibeba timu zao katika mchezo wa ijumaa kwa kuwa hadi sasa wanaonekana kuwa vizuri katika michuano.
Safu ya kiungo ya Ufaransa ni nzuri lakini inacheza faulo nyingi jambo hilo linaweza kuwatatiza kama hawatabadilisha mbinu za kuwazuia viungo wajanja na wenye maarifa wa Ujerumani. Timu zote zinataraji kuonesha kitu tofauti na kile ambacho walikionesha katika michezo iliyopita. Ufaransa vs Ujerumani, Mshindi