maxtrn
Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezini jana asubuhi Coco Beach
Na Baraka Mpenja, Dar e salaam
MAKAMU bingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu uliopita, Dar Young Africans imeanza mawindo ya msimu ujao unaotarajia kuanza mwezi agosti mwaka huu chini ya kocha mpya Mbrazil, Marcio Maximo.
Maximo mwenye heshima kubwa nchini baada ya kuiongoza Taifa stars miaka minne iliyopita aliongoza mazoezi ya Yanga kwa mara ya kwanza jana katika Ufukwe wa Koko Beach.
Katika mazoezi hayo, jumla ya wachezaji 14 kutoka timu ya wakubwa walihudhuria na kufanya mazoezi ya kusaka pumzi na kujenga mwili.
Wachezaji waliofanya mazoezi chini ya Maximo mwenye msimamo wa falsafa yake na nidhamu ni Ally Mustafa “Barthez” , Juma Abdul, Swaleh Abdallah, Rajab Zahir, Mbuyu Twite, Salum Telela, Omega Seme, Hassan Dilunga, Said Bahanuzi, Andrey Coutinho, Hussein Javu, Juma Kaseja, Nizar Khalfani, na Jerson Tegete. 
Katika mazoezi ya jana Maximo aliendelea kuwakosa wachezaji 11 ambao wapo katika timu za Taifa wakijiandaa na mechi za mwishoni mwa mwezi huu kusaka tiketi ya kushiriki fainali za mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.
Wachezaji walio kwenye timu ya Taifa Tanzania ni Deo Munish “Dida”, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub “Cannavaro”, Saimon Msuva, Mrisho Ngasa, Pato Ngonyani, Said Juma huku Uganda ikiwa na Emmanuel Okwi, na Hamis Kizza na Rwanda Haruna Niyonzima.
Countinho aliyesajiliwa kutoka nchini Brazil alitazamwa kwa mara ya kwanza na baadhi ya mashabiki waliojitokeza katika mazoezi hayo.
Jana jioni Yanga iliendelea na mazoezi yake katika uwanja wa Bandari uliopo Tandika jijini Dar es salaam.
Maximo anatarajia kuleta mafanikio katika klabu yake ya Yanga hasa kuboresha mfumo wa soka la vijana.
Enzi zake akiwa Taifa stars, Mbrazil huyu aliinua vipaji vya wachezaji vijana wakiwemo Jeryson Tegete na Kigi Makassi.
Maximo alisema nia yake ni kuifanya Yanga kuwa tishia Tanzania na barani Afrika.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=2958#sthash.quLEjwYx.dpuf
 
Top