Bosi mpya: Louis van Gaal alifanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari leo tangu ajiunge na Manchester United.
LOUIS van Gaal amesema Manchester United ni klabu kubwa duniani, lakini inatakiwa kujijenga upya baada ya kuvurunda msimu uliopita.
Van Gaal amefanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu ajiunge na Man United baada ya kumaliza nafasi ya tatu ya kombe la dunia akiwa na timu ya Taifa ya Uholanzi.
Mholanzi huyo ameisifu klabu ya United kuwa ni kubwa katika ulimwengu wa soka, lakini aliwakumbuksha mashabiki kuwa maboresho ya haraka yanahitajika ili kuepukana na majanga waliyokumbana nayo msimu uliopita.
“Msimu uliopita mlikuwa wa saba, kwahiyo ninyi sio klabu kubwa. Mnatakiwa kujithibitsha wenyewe,” alisema.
“Lakini dunia nzima watu wanaizungumzia Manchester United-hiyo ndio tofauti”.
“Ni changamoto kubwa kwasababu ya hilo na ndio sababu ya kuichagua klabu hii”.
“Nimezifundisha Barcelona, Ajax na Bayern Munich ambazo ni za kwanza katika mataifa yao. Kwasasa nipo Manchester United ambayo ni namba moja nchini England.
“Sijawahi kufanya kazi ligi kuu ya England na hiyo ndio changamoto kubwa”
“Nilipofanya kazi Barcelona, ile ndio ilikuwa ligi bora.
“Nilipofanya kazi Ujerumani, ile ndio ilikuwa ligi bora.
“kwasasa nafanya kazi hapa, labda ndio ligi bora”.
Bosi huyo mpya amegoma kutaja wachezaji wapya atakaowasajili, lakini amesema anataka kukipa nafasi kikosi cha sasa kumuonesha kazi nzuri,
“Njia yangu huwa ni ile ile-nataka kuwaangalia wachezaji nilionao sasa,” alisema.
“Nataka kuona katika wiki ya kwanza kama wanaonesha kitu. Labda hapo ndio nitanunua wachezaji wengine. Shaw na Herera tayari walikuwa kwenye orodha. Niliwapa ruhusu kwasababu ninawapenda.
“Nataka kuona wachezaji wa sasa wanacheza katika falsafa yangu”.
Van Gaal alikataa kuzungumzia nafasi ya Man United, lakini anaamini anaweza kuirudisha katika nafasi yake.
“Nitafanya kazi kadiri niwezavyo, lakini siwezi kutabiri. Hii ni klabu kubwa duniani. Ukiangalia maisha ya kazi yangu, unaweza kuona nilichoshinda”
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=3618#sthash.lMyaMFLO.dpuf