JUAN Mata anaamini ataendelea kumiliki namba 10 katika klabu yake ya Manchester United chini ya kocha mpya, Louis van Gaal.
Mhispania huyo imeichezea Man United mechi 15 na kufunga mabao sita baada ya kusajiliwa kwa dau la paundi milioni 37 kutokea kwa wapinzani wao wa ligi, Chelsea, mwezi januari mwaka huu.
Baada ya kupewa nafasi kubwa ya kucheza chini ya David Moyes msimu uliopita, Mata amekuwa akicheza zaidi nyuma ya Robim Van Persie na Wayne Rooney na wakati huu Van Gaal akitekeleza mfumo wake wa 3-4-1-2 katika dimba la Olf Trafford, nyota huyo atafurahia zaidi nafasi hiyo.
Mata anaamini kurudi katika nafasi yake asilia kutamfanya acheze soka la kiwango cha juu na kuisaidia timu yake kutoka katika nafasi ya 7 waliyomaliza msimu wa 2013-14.
“Naamini nafasi hiyo itakuwa kamili kwangu,” aliwaambia Daily Mail.
“Ninajisikia vizuri katika nafasi ile. Ninaweza kucheza kama kiungo wa ulinzi au kama kiungo wa ushambuliaji, hivyo ndivyo natakiwa kufanya”
“Lakini malengo yangu ni kusaidia kufunga. Naweza kufanya hivyo kwa kucheza nafasi hii na naamni nitakuwa na msimu mkubwa. Lakini kitu cha muhimu zaidi ni msimu kuwa mzuri kwa timu nzima”