Washirika: Mkataba wa Chelsea na Samsung juu ya udhamini wa jezi unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
INAFAHAMIKA kuwa shirika la ndege la nchini Uturuki (Turkish Airlines) linapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya udhamini wa Chelsea kutoka kwa wadhamini wa sasa, Samsung.
Mkataba wa Samsung kudhamini jezi ya Chelsea unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
Shirika hilo kubwa la ndege barani ulaya ambalo linawadhamini nyota wa soka, Lionel Messi na Kobe Vryant, siku za karibuni limeidhamini Barcelona, Manchester United na timu ya Taifa ya Uturuki.
Samsung wameidhamini Chelsea tangu mwaka 2005 chini ya Mkurugenzi mkuu wa zamani Peter Kenyon ambaye alisema klabu itaitangaza vizuri rangi ya bluu duniani.
Chelsea waliongeza mkataba wa udhamini wa jezi yao na Samsung mwaka 2013, lakini wadau wengi wa soka hawakufahamu sana kwasababu haikutangazwa.