Siku zijazo: Manchester United  bado wanaiwinda saini ya  Arturo Vidal (pichani juu)
MANCHESTER United bado hawajamaliza matumizi makubwa ya fedha katika dirisha la usajili.
Katika dirisha dogo la usajili mwezi januari mwakani wametenga paundi nyingine milioni 50  kwa ajili ya kunasa saini za wachezaji wengine.
Tayari United imeshatumia paundi milioni 150 katika dirisha la usajili majira ya kiangazi jumlisha kumsajili Radamel Falcao.
Arturo Vidal, Mats Hummels na Sami Khedira ndio wachezaji wanaowaniwa zaidi na United.
Jaun Mata Garcia atauzwa mwezi januari kama sehemu ya kuongeza wachezaji wapya ili kuimarisha kikosi cha Louis van Gaal.
Pia kuna taarifa kuwa mwanasoka bora wa dunia na Ulaya, Cristiano Ronaldo anaweza kurejea Manchester United.
Nyota huyo anayekipiga Real Madrid ana mapenzi makubwa na klabu yake hiyo ya zamani na anasema anaipenda toka moyoni.
Atletico Madrid, Roma na Juventus  zipo tayari kumsajili Mata aliyesajiliwa na United kutoka Chelsea mwezi januari kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 37.
United inatarajia kukubali ofa ya paundi milioni 20.

 
Top