KESI inayomhusu mshambuliaji, Mganda Emmanuel Okwi inasikilizwa muda huu na kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania.
Habari za ndani zinaeleza kuwa mvutano wa kisheria ni mkali kuhusu kesi hiyo inayosikilizwa katika Hoteli ya Colosseum iliyopo jijini Dar es salaam.
Hata hivyo inasemekana maamuzi yatafikiwa leo hii kama mvutano huo utafikia tamati.
Okwi alisaini mkataba mfupi wa miezi sita na klabu ya Simba kwa madai ya kulinda kiwango chake wakati ikiwa na kesi na klabu yake ya Yanga.
Lakini uongozi wa Yanga unadai nyota huyo aliyeichezea Simba jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ni mchezaji wao na amebakiza mkataba wa miaka miwili.
Baada ya kuona Okwi amesaini mkataba na Simba, Yanga walichokifanya ni kuandika baruaTFF juu ya suala hilo na kuomba kulipwa fidia ya US Dollar 500,000 (sawa na TZS 800,000,000/=) kutoka kwa klabu ya Simba, wakala wake na mchezaji mwenyewe aliongeza.