'Real Madrid asked me not to play in the World Cup final so I tore up the letter' - Di Maria
Karudi mzigoni: Angel di Maria amedai Real Madrid walimtumia barua katika siku ya mwisho ya fainali za kombe la dunia 
ANGEL di Maria amedai kuwa Real Madrid walimuamuru asicheze mechi ya fainali ya kombe la dunia dhidi ya Ujerumani.
Nyota huyo wa Manchester United aliyesajiliwa majira ya kiangazi kwa dau la paundi milioni 60 na kuvunja rekodi ya usajili nchini England amemlaumu rais wa Real Madrid, Florentino Perez kwa kumuondoa katika michuano ya ulaya, akisisitiza kuwa hakuwa na nia ya kuondoka majira ya kiangazi mwaka huu.
Di Maria alikuwa hatari kukosa mechi ya fainali ya kombe la dunia dhidi ya Ujerumani mwezi julai mwaka huu kwa majeruhi ya mguu, na ameweka wazi kuwa maamuzi ya yeye kutoikosa mechi hiyo yalifanywa na kocha wa Argentina, Alejandro Sabella, lakini Real Madrid walimuandikia barua wakimshauri asichezea.
Return: Manchester United's Di Maria was subsequently sidelined in the World Cup final defeat by a thigh injury

 
Top