10703513_10205038845117943_7410317839734433526_n
Afisa habari wa Yanga sc, Baraka Kizuguto (wa kwanza kushoto) Jaja (katikati) na Mbuyu Twite (kulia)baada ya kushinda 3-0 dhidi ya Azam fc jioni ya leo 
katika mchezo wa leo ngao ya jamii yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono dhidi ya matajiri wa jiji timu ya azam kwa mabao matatu kwa bila.magoli mawili ya yanga yalifungwa na mbrazili jaja
5 (1)
Kama kawaida Jaja na uzito wake alianza mdogo –mdogo katika kipindi cha kwanza na kuonekana kutokuwa na uwezo mzuri, lakini timu zilipoenda mapumziko kwa suluhu ya bila kufungana, kocha wa Yanga, Mbrazil, Marcio Maximo alimuelekeza nini cha kufanya.
Dakika ya 58’ kipindi cha pili, Jaja aliitendea haki pasi ya winga mwenye kasi kubwa, Saimon Msuva na kuutia mpira nyavuni na kuiandikia Yanga bao la kuongoza.
Mashabiki wa Yanga walilipuka kwa shangwe, nderemo na vifijo kutokana na bao hilo la Jaja na kusahau kuwa ndiye yule  baadhi yao walikuwa wanamlalamikia.
Wakati mashabiki wakiwa na furaha kubwa, Jaja aliandika bao lingine katika dakika ya 66 ya kipindi hicho na kugeuka mfalme akishangiliwa kwa nguvu zote.
Baada ya kumaliza kazi yake aliyotumwa na Maximo, dakika ya 79, aliitwa benchi  na nafasi yake ikachukuliwa na Hussein Javu.
Katika dakika hiyo hiyo, Haruna Niyonzima alitolewa na nafasi yake ikachukuliwa na Mganda Hamis  Friday Kiiza.
Dakika ya 88 kipidi hicho cha pili, Saimon Msuva aliandika bao la tatu na kuzamisha kabisa ndoto za Azam fc kutwaa kikombe cha Ngao ya Jamii kwa mara ya kwanza.
Baada ya kuingia kwa bao hilo, wachezaji wa Azam walionekana kutoamini na kulowa kabisa.
Hata hivyo mabao mawili waliyofungwa kabla na Jaja yaliwafanya wapunguze matumaini na kushindwa kucheza mpira wao uliozoeleka.

 
Top