DSC_1032
 
kocha phiri
Mshambuliaji wa Simba, Mkenya, Paul Kiongera amewatandika magoli mawili ndugu zake  Gor Mahia, Mnyama akishinda 3-0 jioni.
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WEKUNDU wa Msimbazi Simba wamefanikiwa kuwatungua mabao 3-0 mabingwa wa ligi kuu nchini Kenya (KPL),  Gor Mahia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliomalizika jioni hii ndani ya dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Bao la kwanza la Simba lilifungwa katika dakika ya 55 kipindi cha pili na mshambuliaji mpya kutoka Kenya, Paul Kiongera baada ya kumalizia pasi murua iliyochongwa na Mganda, Emmanuel Anord Okwi.
Okwi aliendelea kufanya vitu vyake ambapo katika dakika ya 73 alipiga shuti kali lililotemwa na kipa wa Gor Mahia, Patrick Odhiambo na mpira kumkuta Ramadhan Singano ‘Messi’ aliyefanya kweli na kuzamisha mpira nyavuni na kuandika bao la pili.
Simba waliendelea kuonesha kiwango kizuri na kulisaka lango la Gor Mahia na katika dakika ya 77 waliandika bao la tatu kupitia kwa Paul Kiongera.
Baada ya kufungwa kwa bao la tatu baadhi ya mashabiki wanaokalia jukwaa la kusini mwa uwanja wa Taifa  na waliokuwa wanaishangalia Gor Mahia walianza kuondoka uwanjani.
Hii unaweza kuitafsiri kuwa waliduwazwa na kiwango cha Mnyama aliyeonekana kuwa na makali katika mchezo wa kwanza wa kimataifa wa kirafiki tangu arejea kocha Phiri.
Okwi ambaye usajili wake bado unaonekana kuwa na utata kwasababu timu yake ya zamani ya Yanga inadai ina mkataba aliitwa benchi na Phiri katika dakika ya 79  na alipewa mkono wa pongezi kwa kazi nzuri, huku mashabiki wa Simba wakishangilia kwa nguvu.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi wa kati, Mathew Akrama kutoka mwanza, mashabiki wa Simba waliofurika uwanjani walikuwa na amsha amsha za muda mrefu kutokana na kandanda lililokuwa likitandazwa na vijana wa Patrick Phiri.
Mashabiki hawakujaa uwanjani, lakini walitosha kwa mechi kama hii ya kirafiki na sababu kubwa ni namna klabu ya Simba ilivyozidi kuimarika chini ya Mzambia Phiri.
Kiufundi Simba wameonekana kubadilika kiuchezaji wakiwa na kasi nzuri, pasi za uhakika na mbinu za kutosha kulifikia lango la mpinzani.
Wakiwa katika kambi ya Zanzibar, Phiri alitumia muda mwingi kuwafundisha wachezaji wake namna ya kukaba kwa usahihi, kupiga pasi za uhakika, kumiliki mpira na kushambulia kwa nguvu.
Mbinu sahihi za Phiri katika mambo haya muhimu yamewafaidisha Simba na wameonekana kucheza mpira wa kufundishika na kupiga mabao matatu kama waliyofungwa na Zesco United katika mechi ya Tamasha la Simba, Agosti 9 mwaka huu katika uwanja huo huo.
Ramadhani Singano ‘Messi’, Paul Kiongera, Okwi, Uhuru, Juma Awadh walionekana kuonana vizuri uwanjani na hata Shaaban Kisiga alicheza soka la kuvutia.
Raphael

 
Top