Wiki moja kabla ya mahasimu wa soka nchini, Simba SC na Yanga SC kukutana katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania Bara, Vodacom Primier League, 2014/15, tayari Bodi ya ligi limemtanga mwamuzi, Israel Mujuni Nkongo kuchezesha mchezo huo ambao hubeba hisia za watu wengi ndani na nje ya Afrika Mashariki.
Simba na Yanga zitakutana katika uwanja wa Taifa, mwishoni mwa wiki ijayo katika mchezo wa kwanza msimu huu. Nkongo alichezesha ‘ pambano la aina yake’ la mahasimu hao msimu uliopita walipotoka sare ya kufungana mabao 3-3, Oktoba 20, 2013 na baada ya kuonyesha kiwango kikubwa Bodi ya Ligi imeweka wazi majina ya waamuzi watakaochezesha mechi hiyo hadharani.
Silas Mwakabinga, ambaye ni mtendaji mkuu wa Bodi ya ligi ( TPL) amewataja Nkongo, Ferdinand Chacha, na John Kanyenye kama ‘ mapilato’ wa mchezo huo utakaopigwa Oktoba 18 katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku mwamuzi wa akiba akiwa Hashim Abdallah, huku Salum Kikwamba akiwa Kamishna wa mchezo huo.
Nkongo amekuwa akitiliwa shaka na timu zote hizo kwa madai ya kuchezesha chini ya kiwango, lakini uamuzi wa Bodi ya Ligi kumpatia nafasi hiyo umekuja baada ya kukimbia uwanjani muda wote huku akisimamisia na kutafsiri sheria za soka kwa usahihi wakati alipopewa nafasi hiyo ya ‘ lawama’ mwaka mmoja uliopita.
akiongea na daily new CEO wa TPLB
"Tanzania Premier League Board (TPLB) Chief Executive Officer (CEO), Silas Mwakibinga, was quoted by the Daily News saying that Nkongo will take charge of the eagerly awaited Dar derby earlier set for Saturday but was postponed to next Sunday to allow the national team, Taifa Stars, to take on Benin’s The Squirrels in an international friendly on a FIFA date. Mwakibinga said TPLB has appointed Nkongo to officiate the match as he is currently among the best referees in the country holding a FIFA badge and deserves to handle the battle of the titans -- the most sensitive in the 14-team league.