Katika kujiandaa na mchezo dhidi ya
Yanga, klabu ya Simba inatarajiwa kucheza na moja ya klabu nchini South Africa.
Kwa mujibu wa taarifa nilizonazo
Simba itajitupa uwanjani siku ya jumamosi kucheza na Orlando Pirates katika
uwanja wa nyumbani wa timu hiyo ya kwa madiba.
Simba iliondoka nchini jana jioni
kwa kutumia shirika la ndege la Fast Jet huku baadhi ya wachezaji wake wakiwa
wameachwa kutokana na kuwemo kwenye majukumu ya timu zao za taifa.