Simba yapaa kwenda Sauzi.
IKIWA zimebaki wiki mbili kabla ya mahasimu wa jadi katika soka la Tanzania kukutana klabu ya Simba inaondoka leo kuelekea Afrika Kusini kupiga kambi ya wiki moja na nusu kujianda na pambano hilo lililopangwa kufanyika Oktoba 18 uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Wakati Simba ikienda Afrika Kusini wapinzani wao Yanga bado hawaja weka wazi sehemu gani watakapokwenda kupiga kambi kujiandaa na pambano hilo lenye upinzani mkubwa kwa soka la Tanzania.
Makamu wa Rais wa Simba Godrey Nyange Kaburu,ameiambia Goal kwamba timu hiyo itaondoka na wachezaji wake wote akiwemo kipa Ivi Mapunda na watafanya mazoezi magumu ili kuweza kushinda mechi hiyo ambayo inaumuhimu mkubwa licha ya kuwa na matokeo mabaya katika mechi zilizo pita.
“Kilikitu kinakwenda sawa ikiwemo kuandaa Paspoti na viza za kuingilia Afrika Kusini matumaini yetu kambi ya Afrika Kusini itakuwa ya mafanikio na kupata ushindi kama tulivyo dhamiria,”amesema Kaburu
Simba imekuwa na mwenendo mbaya tangu kuanza kwa ligi ya msimu huu na ina pointi tatu katika mechi tatu ilizocheza ikiwa nyumbani uwanja wa taifa ambazo zote imeambulia sare huku wapinzani wao Yanga wakiwa na pointi sita na wanashika nafasi ya tatu nyuma ya Azam na Mtibwa Sugar inayoongoza ligi.
 
Top