BAADA ya timu yake kupoteza mechi mbili mfululizo, kocha msaidizi wa Azam FC Kalimangonga Ongola ameamua kubwaga manyanga.
Azam FC, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanania Bara (VPL), wamepoteza mechi mbili mfululizo za ligi hiyo baada ya kucheza mechi 38 bila kupoteza hata moja, wakifungwa 1-0 nyumbani dhidi ya JKT Ruvu kabla ya kufungwa 1-0 ugenini dhidi ya Ndanda FC Jumamosi.
Jaffari Idd Maganga, msemaji wa Azam FC ameuambia mtandao huu jijini Dar es Salaam leo kuwa kocha huyo ameamua kujiuzulu ili akaongeze elimu zaidi ya ukocha nje ya nchi.
“Ongala ameamua kuachia ngazi ili apate muda mzuri wa kuongeza elimu ya ukocha nje ya nchi. Tumemshukuru kwa mchango wake mkubwa akiwa mchezaji na kocha wa Azam FC,” amesema Jaffari.
Azam FC inayonolewa na Macameroon Joseph Omog, itaanza kukosa huduma za Ongala katika mechi ya wikiendi hii ambayo watawakabili mabingwa wa 1988 wa Tanzania Bara, Coastal Union kwenye Uwanja wa Azam jijini Dar es Salaam.
 
Top