FC Barcelona v Getafe CF - La LigaMaisha yanakwenda kasi kama mwanga, Upepo wa umebadilika ghafla kwenye maisha ya Lionel Messi miaka mitatu hadi minne iliyopita ungemuuliza Messi unafikiria kuihama Barcelona angekujibu hapana sifikirii kwa kuwa nataka kumalizia soka langu kwenye viunga vya Catalunya.
Lakini juzi Messi aliulizwa juu hatma yake ya maisha kupitia gazeti la Ole la nchini Argentina, alijibu hajui hatma yake ndani ya Barcelona, pia  msimu huu unaweza ukawa ndio msimu wake wa mwisho ndani ya klabu hiyo.
Unajua ni kwanini anataka kuondoka? Tangu  kuonndoka kwa utawala wa Juan Laporta na kuja utawala wa Sandro Rosell kumebadilisha Maisha ya Messi hata Rosell alipoachia ngazi na kuja utawala wa rais wa sasa Josep Sandro Batromeu bado Messi anaonekana hana jipya chini ya tawala za sasa za Barcelona.
                Bartomeu: Messi is happy at Barcelona
Messi hana furaha toka ulipoondoka utawala Laporta, kwasababu hata moja ya sababu iliyopelekea kuondoka kwa kocha Pep Guardiola ni kutopewa ushirikiano mzuri toka kwa utawala wa Sandro Rosell , chini ya utawala wa Laporta na benchi la ufundi la Guardiola, Messi alipewa kile alichotaka na timu ilijengwa kumzunguka yeye na ndio maana Guardiola alimletea Messi msaidizi kama Alexis Sanchez yote ni kumfanya Messi awe huru kwenye mfumo wa x mass tree.
Chini ya Utawala wa Rosell alinunuliwa  Neymar sio kama msaidizi wa Messi bali ni mtu ambaye amekuja kuvaa viatu vya Messi, ukiuliza kwanini kaja Neymar utaambiwa Messi hana jipya tena maajabu yake yamezoeleka hivyo hayawafanyi wahudhuriaji wa mpirani waje kwa wingi Nou Camp, ila wanaamini Neymar anaujaza uwanja kwasasa.
Gwiji wa zamani wa Barcelona Johan Cruyff aliwahi kudokeza kuwa itakuwa ngumu kwa klabu kuhimili kuwafanya Messi na Neymar kuishi furaha.
Lakini sababu za kiuchumi pia zinapelekea klabu kushindwa kwenda kasi ya hawa watu wawili na ndio maana Messi kaomba mkataba mpya lakini makamu wa rais wa Barcelona Javier Faus amekaririwa akisema klabu haina mpango wa kumpa mkataba mpya Messi bali klabu inaangalia uwezekano wa kumpa mkataba mpya Neymar.
Timu itaundwa kupitia Neymar na Suarez kaja kumsaidia Neymar mwenye umri wa miaka 21 katika kuijenga Barcelona mpya.
 
Top