IDADI YA MAJERUHI MAN UNITED
Habari hii kwa vyovyote haiwezi kufurahiwa na mashabiki wa Manchester Unted lakini hakuna jinsi zaidi ya kukubaliana na ukweli wake na kusonga mbele kwa imani .
Habari yenyewe ni hii hapa , kumhusu mshambuliaji raia wa Colombia Radamel Falcao ambao inasemeka amepata jeraha lingine ambalo litamfanya akae nje ya uwanja kwa wiki nyingine mbili .
Jeraha hilo ambalo Falcao amelipata kwenye kigimbi cha mguu wake litamfanya mshambuliaji huyo kuukosa mchezo unaofuata kwenye ligi ya England dhidi ya Arsenal .
Hadi sasa Falcao ameanza kwenye michezo mitatu pekee huku akifunga bao moja .
Hadi sasa Falcao ameanza kwenye michezo mitatu pekee huku akifunga bao moja .
Falcao anaendeleza orodha ndefu ya majeruhi wa Man United orodha ambayo inatosha kuunda kikosi cha wachezaji 11 wanaoweza kuingia uwanjani .
Orodha hiyo tayari ina watu kama Marcos Rojo , Rafael Da Silva , Daley Blind , Phil Jones na Johny Evans hali inayomfanya kocha Louis Van Gaal kuwa na idadi ndogo ya wachezaji ambao anaweza kuwachagua kwenye mechi za timu hiyo zinazokuja hivi karibuni .

 
Top