Klabu bingwa ya kandanda nchini, Azam FC imekubali kumuuza mshambulizi wake bora zaidi, Muivory Coast, Kipre Tchetche kwa timu ya Kelntan FC ya nchini Malasyia nafasi ya mshambulizi huyo itazibwa na Mmali, Mohammed Traore. Hii ni kamari ambayo wakati mwingine huzaa hasara kubwa. Timu hiyo imeonekana kushindwa kucheza kitimu zaidi msimu huu tofauti na msimu uliopita chini ya Mwalimu, Stewart Hall lakini kitendo cha kumuuza, Kipre mwenye kasi na kumsaini mchezaji anayetegemea kuletewa mipira tu kinaweza kuifanya timu hiyo kupooza kabisa katika safu ya mashambulizi.
Didier Kavumbagu, John Bocco, Gaudensi Mwaikimba, Leonel Saint wote hawa ni washambuliaji wasio na kasi, Kipre alikuwa na uwezo binafsi katika uchezaji wake, alikuwa akishambulia vizuri kutokea pembeni ya uwanja na alikuwa hatari kutokana na kasi yake. Benchi la ugfundi la timu hiyo linakabiliwa na changamoto kubwa, lakini watalazimika kukubali changamoto kubwa zaidi ‘ kuishi bila msaada wa mabao ya Kipre’ mchezaji ambaye alijiunga na Azam FC miaka minne iliyopita na kushinda tuzo ya ufungaji bora msimu wa 2012/14 huku akishinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu uliopita.
Azam ina kila kitu, ni timu ambayo ipo chini ya mtu Fulani hivyo kocha Joseph Omog anakabiliwa na mtihani mkubwa kwa kuwa timu hiyo itacheza michuano ya klabu bingwa baadae mwakani. Wiki iliyopita timu hiyo ili msaini mlinzi raia wa Ivory Coast, Serge Paschal Wawa kutoka El Merreikh ya Sudan Kaskazini. Azam inahitaji kuendana na mabadiliko ya kweli kama wanataka kushindana na timu kama, TP Mazembe au klabu yoyote kubwa barani Afrika. Kubadilisha mfumo wa uchezaji ambao umeonekana katika michezo saba msimu huu ni jambo lisiloweza kuepukika, vinginevyo wataanguka.
Azam inahitaji mabadiliko, lakini si kuwauza wachezaji muhimu kama Kipre. Nafikiri benchi la ufundfi linahitaji kufanya jitihada kubwa katika kipindi cha miezi miwili kuelekea michuano ya klabu bingwa kama kweli wanahitaji kufanya vizuri katika michuano hiyo ambayo watashiriki kwa mara ya kwanza. Kumuuza Kipre na kumsaini, Traore ambaye aling’ara katika michuano ya Kagame Cup, Agosti mwaka huu nchini Sudan ni kamari ambayo mchezeshaji wake ni Omog.
Azam itakuwa ikicheza mchezo wa polepole sana. Kwa namna yoyote ile timu hiyo itacheza hivyo, jambo ambalo linaweza kuwaletea ugumu katika michuano ya kimataifa ambayo huitaji pia wachezaji wenye ufundi na kasi wawapo uwanjani. Katika machaguo ya Lieonel, Kavu, Bocco, Mwaikimba na Traore, Azam haitakuwa tishio katika ufungaji wa mabao kwa kuwa watahitaji viungo wenye uwezo mkubwa zaidi ili kuichezesha safu ya mashambulizi isiyo na 
 
Top